HabariMichezo

Ronaldo afikisha goli 500, akitupia nne peke yake

Mchezaji wa Al-Nassr, Cristiano Ronaldo amefikisha magoli 500 ngazi ya Klabu kwenye maisha yake ya soka.

Ronaldo amefikisha goli la 500 hapo jana usiku baada ya kufunga goli nne (4) peke yake kwenye mchezo uliyomalizika 4-0 dhidi ya Al-Wehda katika Saudi Pro League.

Kwa sasa Ronaldo ana jumla ya goli 503 ya katika Klabu tano tofauti za Ligi Kuu. Magoli 103 akiwa na Manchester United, 311 Real Madrid, 81 na Juventus, matatu (3) na Sporting Lisbon, na kwa sasa matano (5) Al Nassr.

Mreno huyo ambaye Jumapili ya Februari 5, alitimiza umri wa miaka 38 ameyafunga magoli hayo manne na kuwapatia Al-Nassr ushindi.

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents