Michezo

Rosberg amefanikiwa kumaliza namba 1 katika mbio za Japan Grand Prix

Katika kufuzu mbio za Japan Grand Prix usiku wa kuamkia leo, Mjerumani Nico Rosberg amefanikiwa kumaliza namba 1 akimpita dereva mwenzake wa Mercedes Lewis Hamilton kwa sekunde 0.013, namba 3 amekamata Kimi Raikonnen wa Ferrari.

3935279400000578-3828211-image-a-29_1475912491811

Hii inakuwa mara ya 3 mfululizo Nico anashika namba 1 katika kufuzu mbio hizo za Japan lakini hajawahi kushinda hata mara 1 licha ya kuanza katika Pole Position.

Lewis Hamilton kesho katika mbio hizo atakuwa anatafuta ushindi wake wa 3 mfululizo wa Japan Grand Prix baada ya kushinda mwaka 2014 na 2015 ambapo pia hakuanza katika Pole Position.

Nico Rosberg bado anaongoza msimamo wa madereva akimpita Lewis Hamilton kwa pointi 23 huku zikiwa zimebaki Grand Prix 5.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents