Habari

Rufaa ya Sabaya yaja na sababu 10

Wakili wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Lengai Ole Sabaya ameweka wazi kuwa tayari wameshakata rufaa dhidi ya hukumu ya miaka 30 aliyopatiwa Sabaya na wenzake.

Wakili namba moja wa Sabaya, Mosses Mahuna

Akizungumza nje ya mahakama, Wakili namba moja wa Sabaya, Mosses Mahuna amesema rufaa walishaifikisha mahakama ya rufaa na imepewa Na.129/2021.

Amesisitiza kwamba utetezi sababu zisizopungua 10 kuweka mapingamizi kwenye hukumu hiyo iliyotolewa Oktoba 15 mwaka huu, ambapo Sabaya na wenzake wawili walihukumiwa kifungo cha miaka 30.

Akizungumzia afya ya Sabaya ambaye ameshindwa kufika mahakamani kwa siku ya tatu leo, Mahuna amesema hali ya mteja wake bado siyo nzuri kwani anasumbuliwa na tumbo pamoja uti wa mgongo kutokana na ajali aliyoipata akiwa katika majukumu yake kabla ya kufungwa.

Akizungumzia suala la mteja wake kupelekwa hospitali kutokana na ugonjwa, Wakili Mahuna amesema suala hilo wanahusika nalo Jeshi la Magereza.

Kwa upande wa kesi ya Na. 27/2021 uhujumu uchumi inayomkabili Sabaya na wenzake sita imeahirishwa mpaka Novemba 15, 2021 ambapo Jamhuri itaendelea kutoa ushahidi.

BY: Fatuma Muna

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents