Habari

Rwanda kuwapa hifadhi wasichana wa shule kutoka Afghanistan

Rwanda itakuwa mwenyeji wa wasichana wengi wa shule wanaohamishwa kutoka Afghanistan kufuatia kuchukuliwa kwa nchi hiyo na wanamgambo wa Taliban.

Shabana Basij-Rasikh, mwanzilishi wa Shulebinafsi ya Uongozi Afghanistan (SOLA) Jumanne alisema wanafunzi wapatao 250, wafanyikazi na wanafamilia walikuwa njiani kwenda Rwanda, kupitia Qatar, kuanza “muhula mwingine kwa wanafunzi wote’

Wizara ya elimu ya Rwanda ilituma ujumbe wa kukaribisha jamii ya SOLA nchini:

Mwanzilishi wa shule hiyo alisema walikuwa na matumaini ya kuishi kwa muda tu hadi muhula ukamilike na kurudi Afghanistan wakati hali itakapokuwa tulivu .

Waafghani wamekuwa wakikimbia kuondoka nchini mwao, kwa hofu ya kuishi chini ya utawala wa Taliban, na maelfu wamehamishwa kwenda nchi zingine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents