Michezo

Samuel Eto autaka urais wa shirikisho la soka nchini kwao Cameroon

Nyota wa mpira wa soka nchini Cameroon Samuel Eto atangaza kugombea urais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Cameroon. Tangazo hilo limetolewa Jumanne katika kurasa zake za mitandao ya kijamii.

“Nimeamua kuchukua uamuzi huu kwasababu ya kuipenda Cameroon na kupenda soka yetu”, alielezea Samuel Eto katika taarifa yake.

Aliandika pia, “ni wakati wa kujenga upya mpira wetu”. Baada ya uvumi kadhaa, Eto ameamua kuwa mgombea wakati kuna utata juu ya marufuku ya uraia mara mbili nchini Cameroon.

Samuel Eto alikuwa raia wa Uhispania wakati alikuwa akichezea Uhispania.Miongoni mwa masharti yanayotakiwa kuwa mgombea wa urais wa shirikisho la mpira wa miguu la Cameroon, ni marufuku ya kuwa na utaifa wa kigeni.

Samuel Eto ni kigogo wa tatu wa zamani kugombea urais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Cameroon.

Hata hivyo, bado haijulikani ikiwa ugombea wake utathibitishwa. Uchaguzi umepangwa kufanyika Desemba 11.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents