Seneta wa upinzani auawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana Cameroon

Seneta wa upinzani ameuawa kwa kupigwa risasi Magharibi mwa Cameroon ambako uasi wa umwagaji damu unafanywa na wanaharakati wanaopigania kujitenga. Seneta Henry Kemende, ambaye mwili wake ulipatikana jana, aliuawa usiku na watu wasiojulikana ambao walikuwa na silaha.

Alikuwa wakili na seneta wa chama cha Social Democratic Front – SDF, mojawapo ya vyama vya upinzani Cameroon. Chama chake kimesema gari alilokuwa analitumia wakati wa shambulizi hilo limetoweka.

Mpaka jana hakuna yeyote aliyejitokeza kudai kuhusika na mauaji hayo. Cameroon imekumbwa na machafuko tangu Oktoba 2017, wakati wapiganaji walitangaza taifa huru katika eneo la kaskazini magharibi na kusini magharibi, eneo lenye jamii ya walio wachache wanaozungumza kiingereza katika nchi yenye watu wengi wanaozungumza Kifaransa. Cameroon kwa sasa ni mwenyeji wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.

Related Articles

Back to top button