Burudani

Serengeti Fiesta kufanyika leo Shinyanga

Baada ya kufanya maonyesho ya kuvutia katika zaidi ya mikoa sita nchini, Serengeti Fiesta inaendelea Ijumaa hii mjini Shinyanga.

fiesta2014

Onyesho la Serengeti Fiesta mjini humo lilipaswa kufanyika Septemba 6 mwaka huu kwenye Uwanja wa Kambarage, lakini likaahirishwa kutokana na ajali mbaya iliyotokea mkoani Mara ikihusisha magari matatu. Wakazi wengi wa Shinyanga wamefurahia na kuipongeza timu nzima ya SBL kwa kujitolea kushirikiana na jamii wakati wa ajali hiyo iliyoua karibu watu 40, na kuzitaka kampuni nyingine kuiga mfano huo.

Timu ya SBL pamoja na wasanii waliwatembelea majeruhi hospitalini na kuzifariji familia zilizopoteza wapendwa wao, ambapo walichangia chakula na vitu vingine muhimu. Katika kuonyesha kuwa SBL ipo nyuma ya kaulimbiu ya mwaka huu ya Serengeti Fiesta isemayo; ‘SambazaUpendo’, mapato ya mlangoni kwenye onyesho la Serengeti Fiesta 2014 mjini Musoma, yalipelekwa kwa familia zilizoathirika na janga lile la ajali.

Young Killa, Fid Q na Stamina wakiongozana na zaidi ya wasanii wengine 10 wenye vipaji vya hali ya juu, wameahidi kufanya onyesho la nguvu kwenye Uwanja wa Kambarage. Orodha ya wanamuziki hawa inawajumuisha pia akina Ommy Dimpoz, Linah, Recho, Ney wa Mitego, Chege na Temba, Nikki II, Mo Music na Kadja, ambao watasindikizwa na wasanii wenyeji wa mkoa wa Shinyanga.

Baada ya Shinyanga, Serengeti Fiesta 2014 itakuwa njiani kuelekea Geita ikiwa ni mwendelezo wa maonyesho 18 yaliyoahidiwa kwa mashabiki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents