Habari

Serikali ikiwatumia wasanii inaweza kuwakamata wauza unga?

Madawa ya kulevya yamekuwa ni janga kubwa la dunia, vijana wengi wameathirika na wengine wamepoteza maisha kutokana na matumizi hayo.

Babu Tale, Chidi Benz na Kalapina

Japo janga hili ni la dunia nzima, pia kwenye muziki wa Tanzania ni sehemu moja wapo iliyoathirika vikubwa kutokana na uwepo wa madawa ya kulevya.

‘Vijana ndiyo taifa la kesho’, madawa ya kulevya yamekatisha ndoto nyingi za vijana ambao walionekana kuja kufanya makubwa siku za usoni. Tunamkumbuka marehemu Ngwair, alikuwa ni mkali muziki wa Hip Hop Bongo, pengo lake halijazibika mpaka kesho.

Japo kuna msemo unasema ‘ukimuona mwenzio ananyolewa wewe tia maji’, hakuna anayefikiria hili kwa kuwa binadamu tumeumbwa kwa kusahau. Ray C na Q Chief yaliwatokea makubwa mpaka wakasahaulika kwenye ramani ya muziki, hatimaye walitoka huko kwenye giza nene, lakini kwa habari tunazozisikia kwa Ray C kuhusu sasa hakuna mwenye uhakika nazo.

Wauzaji bado wapo wanaendelea na biashara zao, je Ray C na Q Chief walishindwa kutoa ushirikiano kwa serikali kuwabaini wauzaji? Siku kadhaa zilizopita Chidi Benz aliwatoa watu wengi machozi, hakuna aliyeamini kuwa anayemuona kwenye TV na picha zilizoenea mitandaoni kama kweli alikuwa ni Chidi.

‘Mficha maradhi kifo humuumbua’, kama wasanii ambao ndiyo kioo cha jamii wanakuwa hivi, je vipi kuhusu vijana mitaani wasiojulikana ambao tunapishana nao kila siku. Kuna kazi kubwa kwa serikali kufanikisha hili.

Njaa ya kuwatumia wasanii waliotumia na wanaotumia madawa inaweza ikawasaidia kuujua ukweli? Baharini kuna dagaa wengi lakini pia papa wapo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents