Habari

Serikali itaendeleza ushirikiano na Umoja wa Mataifa – Mh. Samia

Serikali kupitia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan, imesema kuwa itaendelea kushirikiana na umoja wa mataifa katika kuleta maendeleo, katika sekta za kiuchumi na kijamii, kulinda amani, kuimarisha sekta ya viwanda na kuwahifadhi na kuwahudumia wakimbizi kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika.

Mama Samia ameyaeleza hayo leo Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Karimjee na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan katika maadhimisho ya siku ya Umoja wa Mataifa (UN) ya kutimiza miaka 72 tangu kuanzishwa kwake.

“Umoja wa mataifa umekuwa ukifadhili miradi mingi ya maendeleo hapa nchini, katika kutekeleza malengo yake ya millennium ya umoja huo, hivyo naomba wadau na wafadhili wa maendeleo kutoka umoja huu kuendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania ambayo imekuwa ikishirikiana nao kwa mafanikio makubwa na kutambua jitihada zao katika kuleta maendeleo,” alieleza Mh. Samia.

“Serikali chini ya Mhe. Rais Magufuli inaendelea kupambana dhidi ya rushwa, matumizi mabaya ya rasilimali za umma, wizi wa nyara za serikali na matumizi mabaya ya fedha za umma, serikali pia inatekeleza malengo 17 ya umoja wa mataifa kwa kuongeza matumizi ya rasilimali za ndani, kuongeza makusanyo ya kodi pamoja na kuzuia mianya ya ukwepaji wa kodi,” alifafanua Mama Samia.

Mama Samia aliongeza kuwa serikali imekuwa ikishirikiana na UN katika harakati za kulinda amani katika mataifa mbalimbali barani Afrika kama vile Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo. Vilevile alitoa wito kwa umoja huo kufanya mabadiliko katika baraza la usalama ili kuimarisha ulinzi, amani na ushrikiano dhidi ya makundi ya kigaidi yanayozidi kuongezeka kila uchao.

Makamu wa Rais ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo yaliyokuwa na kauli mbiu isemayo “Maendeleo ya viwanda na utunzaji wa mazingira kwa maendeleo endelevu,”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents