Habari

Serikali kuinufaisha Dar kwa mabasi mengine 165 mapya ya mwendo kasi

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeanza kufanya mchakato wa kuagiza mabasi mapya 165 ya mwendokasi ambayo yatatoa huduma za usafiri kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam ambapo huduma hiyo bado haijafika.

DART

Mtendaji Mkuu wa mradi wa mabasi hayo, Ronald Rwakatare amewaeleza wajumbe wa kamati ya Bunge ya Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa waliotembelea mradi huo kuwa wanatarajia mabasi hayo yataanza kazi Aprili mwakani.

Rwakatare amesema kuwa tayari serikali imeshatangaza zabuni ya kununua mabasi hayo na mwezi Disemba, mwaka huu itasaini mkataba na mzabuni huyo.

“Mabasi haya yatahudumia maeneo ya Morocco, Tegeta, Masaki, Makumbusho na mengine yasiyofikiwa, wakati tukiendelea na ujenzi wa awamu ya pili ya mradi huo,” amesema mtendaji huyo. Mradi wa ujenzi wa barabara wa awamu ya pili unatarajiwa kuhusisha maeneo yenye wakazi wengi na yenye shida ya usafiri ambapo ni kati ya Mbagala na Gongo la Mboto.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents