Habari

Serikali kupeleka umeme vijiji vyote Kibiti

Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imesema kuwa ina mpango wa kupeleka umeme katika vijiji vyote vya jimbo la Kibiti mkoani Pwani.

Hayo yameelezwa leo Bungeni mjini Dodoma, na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Dkt Medred Kalemani wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Kibiti Ally Ungando aliehoji,

Kutoka na mauaji yanayoendelea Wilayani Kibiti bado kuna hitaji umeme, Je serikali ina mpango gani wa kutuletea umeme katika vijiji vilivyobakia?

“Serikali imekusudia kuangaza umeme vijiji vyote nchi nzima, napenda niseme hivyo kwasababu Mheshimiwa Ungando tumeshirikiana sana lakini niseme tu hivi vijiji vyote vya jimbo la Kibiti vitapelekewa umeme sasa kupitia mradi wa REA hadi kufikia mwaka 2021 vijiji vya Kibiti vitakuwa vimeshapata umeme vijiji vyote,” amesema Kalemani.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents