Burudani

Shaa: Nilitamani kuimba Taarab kabla ya kutoa ‘Sugua Gaga’, abatizwa jina la ‘Malkia wa Uswazi’

Muimbaji Sarah Kaisi aka Shaa hivi sasa ana aka mpya ya ‘Malkia wa Uswazi’, iliyotokana na aina ya muziki alioanza kuufanya tokea mwaka jana baada ya kuanza kusimamiwa na Mkubwa Fela pamoja na Babu Tale.

shaa11

Kitu ambacho huenda ulikuwa hufahamu ni kwamba, hata kabla hajatoa ‘Sugua gaga’ wala hajaanza kusimamiwa na mkubwa Fela tayari alikuwa na ndoto ya kujaribu kufanya muziki wa Taarab kipindi bado anasimamiwa na Unity Entertainment ya AY.

“Nilikuwa natamani kujaribu taarab, lakini pale studioni nikiwaambia wananiambia dada hebu tulia kwanza unajua sasa hivi mtu anaekusimamia ni AY”,Amesema Shaa kupitia Magic FM.

“Ndio ile tukatoa wimbo wa Lava Lava, Promise nini…baada ya hapo kama mwenyezi Mungu yaani alivyopanga alivyoandika huwa linatokea mkubwa Fela na Tale wakaja wakasema hivi Shaa hivi unajua huko uswazi vile vile watu wanakukubali. Nikawaambia kaka yaani nimelifikiria lakini sitaki kuingia choo cha kiume […] ni vizuri nyinyi wenyeji sikio lenu liko kitaa mnaweza mkanisaidia vizuri kwamba nifanye muziki gani mi nahamu na taarab wakasema aah tulia kwanza mtoto twende tukupeleke kwenye ‘Sugua gaga’ kwanza”.

Mapokeo mazuri ya single ya ‘Sugua gaga’ licha ya kufanya aongeze mkataba wa mwaka mmoja na uongozi mpya, lakini pia umemuongezea idadi karibia mara mbili ya aliokuwa nao kabla.

“Nadhani katika mitandao ya kijamii nimeongeza asilimia ya mashabiki karibu asilimia 80 ya mashabiki wapya kutokana tu na ile kuhamia kwenye muziki wa nyumbani zaidi, wa kitaa zaidi.”

Shaa kwa sasa ameachia single mpya iitwayo ‘Subira’ iliyoandikwa na Fela na kutengenezwa na producer Shirko, video yake itafuata baada ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents