HabariMichezo

Shabiki aingia kwenye 18 za Bodyguard wa Lionel Messi

Bodyguard binafsi wa Lionel Messi usiku wa kuamkia leo, aliingia uwanjani kwa kasi ya ajabu kama ‘Kipanga’ na kumdaka shabiki mmoja aliyevalia jezi ya Barcelona wakati alipomkaribia staa huyo kwenye mchezo wa LAFC dhidi ya Inter Miami.

Mlinzi huyo anayejulikana kwa jina la Yassine Chueko aliingia na kumdaka shabiki huyo licha ya kuwa wapo walinzi wa uwanja wanaostahili kufanya kazi hiyo.

Yassine Chueko ambaye ni Bodyguard wa mchezaji huyo raia wa Argentina amekuwa akitrendi kwenye Mitandao ya kijamii kutokana na tabia yake ya kumfuata Lionel Messi kwa karibu mno na kila kona.

Kila Messi atakapo inua mguu, Bodyguard anaweka wake, kwamaana ‘Anakaba hadi Kivuli’ hali inayowakosesha raha mashabiki wa MLS ambao wanatamani kumsogelea, Messi ili kupata saini na picha pamoja naye.

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents