Burudani

Shetta aitaja sababu kubwa ya wasanii kufanya video nje ya nchi

Rapper wa ‘Kerewa’, Shetta amesema sababu kubwa inayowafanya wasanii wengi kwenda kufanya video nje ya nchi ni kuepuka gharama kwakuwa sio rahisi kumleta director na timu yake kushoot video nchini.

Akiongea na Bongo5, Shetta amesema msanii anapofanyia video Afrika Kusini ama Uingereza si kwasababu Tanzania hakuna location nzuri, bali ni kwakuwa gharama zinaweza kuwa mara nne zaidi kama video ikifanyika nchini kwa kumtumia muongozaji wa nje.

“Ukitaka kwenda kufanya video nje unawekeza fedha nyingi maana unatoa pesa ambayo director anaitaka almost dola 20,000 – 25,000, hiyo anataka yeye, tu anatimu ya watu zaidi ya 15,” amesema.

Rapper huyo amesema kama yeye au Diamond angeamua kumleta Godfather Tanzania angetumia zaidi ya milioni 100 wakati kwa kufanya video Afrika Kusini, Diamond ametumia zaidi ya milioni 50. Shetta amesema umefika wakati wapenzi wa muziki wa Tanzania wakaacha kuwakatisha tamaa wasanii na badala yake waanguke mkono katika kazi zao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents