Burudani

Shilole: Alikiba una kiburi cha kishamba, Diamond amekugaragaza

Kupitia Insta yake ameandika kuwa:- Hapana jamani, kila siku nakosewa nikitaka kuongea washauri wangu wanasema nikae kimya. HILI NIMEKOSEWA SANA NA SIWEZI KUKAA KIMYA SASA MNANIONEA.

@officialikiba nakushukuru sana leo umeuthibitishia ulimwengu mambo yafuatayo :

1. Una kiburi cha kishamba, unavimba na kupandisha mabega katika namna isiyostahili. Huna utu ambao watu wako wanakupamba kwamba uko nao. Sawa mimi na wewe hatuna mazoea (Hilo ni kweli kabisa), lakini mimi na wewe tupo katika field moja. Ningeweza kuja kwenye shughuli yako kuonesha upendo tu hata kama sijaalikwa, ungekuwa na utu, haikuwa na haja kwenda redio na kusema “SIJAMULIKA” : ili mimi nionekane nilivamia tu shughuli tu?. Shame on you Ali. (ila kwa tabia zile za kwenda Marekani kuomba dada zako naniliu hushangazi)
.
2. Umethibitisha kwamba wewe hauko ‘organized’. Kwa sababu, utasema nilipostiwa kwenye page yako na kutafutwa na watu wako wakati hawajakutaarifu. Kwa hiyo kwa ukubwa tunaotangaziwa unao Bwana Ali, unataka kusema hujui hata kilichopostiwa kwenye page yako rasmi katika siku yako muhimu? Kwa hiyo hata Nasibu uliyeshindana naye miaka mingi akakugaragaza angeweza kualikwa bila wewe kujua? (Nasibu humuwezi tusikudanganye). Wewe ndo msanii wetu wa kimataifa? SIJAPENDA.
.
Kwa ufupi, sikuenda kwenye shughuli kama mvamizi. Nilialikwa, nimescreenshot post yake na kupost hapo juu.

Shughuli ile ya hovyo hovyo na kupoa kama uji wa mngonjwa, ilihitaji uwepo wangu. YEEES, Niliwasaidia kuchangamsha.
.
Katika mazingira ya sasa mimi hakuna lolote ninalofaidika kwa kwenda kwenye shughuli ya Ali, sana sana nilienda kumuongezea followers.
.
Kama nahukumiwa, nihukumuni kwa kupenda shughuli za wenzangu. Kila nikialikwa Zuwena mimi nakweenda kuonesha upendo. NA SITAACHA KUFANYA HIVYO KWA SABABU YA WATU WALIOKOSA UTU NA SHUKRANI KAMA ALI.
.
Aah hasira zimeisha, njooni Shishi Food tule ubwab

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents