Burudani

Shirikisho la muziki na NSSF wamkabidhi mjane wa Gurumo shilingi milioni 2

Shirikisho la Muziki Tanzania, ‘SHIMUTA’ likishirikiana na NSSF wamemkabidhi mjane wa msanii wa muziki, Mzee Muhidin Maalim Gurumo shilingi milioni mbili kama ahadi yao waliyoitoa kipindi cha nyuma.

Mjane wa aliyekuwa msanii wa muziki mzee Gulumo akikabidhiwa hundi ya milioni mbili na afisa mahusiano wa NSSF Juma Kintu
Mjane wa aliyekuwa msanii wa muziki Mzee Gurumo akikabidhiwa hundi ya shilingi milioni mbili na afisa mahusiano wa NSSF Juma Kintu

Akizungumza na waandishi wa habari ndani ukumbi wa Benjamini Mkapa Towers, Rais wa shirikisho la muziki, Addo November amesema walimuaidi mjane huyo kumpatia Bajaj ili iweze kumsaidia kimaisha.

Rais wa shirikisho la muziki i Ado November akizungumza na waandishi
Rais wa shirikisho la muziki Ado November akizungumza na waandishi wa habari

“Hapo mwanzo tulimwaidi mjane tutamnunulia Bajaj ili iweze kumsaidia katika maisha yake,” alisema. “Leo tumetimiza hili tukishirikiana na wadau wetu NSSF. Tumefanikisha kutimiza ahadi kwa kumkabidhi mjane cheki ya milioni mbili. Tumeona tumkabidhi pesa mwenyewe ili ajue kama ataenda kununua Bajaj au pengine anahitaji mahitaji mengine. Kwahiyo tumeona pesa inaweza kumsaidia zaidi.”

Naye mjane wa GuRumo alilishukuru shirikisho la muziki pamoja NSSF ambao wameona umuhimu wa kumsaidia katika kipindi hicho kigumu.

Mjane mzee Gulumo
Mjane mzee Gurumo

“Nawashuku wote, nalishukuru shirikisho la muziki pamoja na mfuko wa jamii NSSF kwa kuniondoa na ukiwa,” alisema.

Mjane wa Gulumo alipkea hundi
Mjane wa Gurumo akipokea hundi


Mmoja kati ya wasanii wakongwe wa muziki wa band akizungumza
Mmoja kati ya wasanii wakongwe wa muziki wa band akizungumza

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents