Michezo

Shuhudia mashabiki wa Liverpoll walivyolishambulia kwa mawe na chupa basi la Real Madrid (+ Video)

Moja ya mashabiki wanaotajwa kuwa wajeuri sana dunaini ni mashabiki wa Liverpool, timu nyingi duniani huwa zinauogopa uwanja wa Anfield sio kwamba una tatizo kubwa sana, uwanja huo unaogopwa na timu nyingi hasa zinazotoka nje ya Uingereza moja kwa sababu timu hiyo inapofika nyumbani huwa inabadilka hata ari inakuwa kubwa lakini la pili mashabiki wa Liverpool hutajwa kama mashabiki ambao huzifanyia timu nyingi sana fujo kama hivyo ambavyo wamefanyiwa Real Madrid siku ya jana.

Kwa Uingereza timu ambayo wana upinzani mkubwa na hata fujo hutokea siku zikikutana na Liverpool na Manchester United na hii ni kutokana na upinzani wao na ndio maana ni mara chache sana kuona mechi ya ligi ya Manchester United dhidi ya Liverpool ikichezwa usiku sana mara nyingi kama sio mchana basi jioni hiyo ni kutokana na mashabiki wa timu zote mbili kuwa na tabia ya kufanyiana fujo hadi kufikia kuwafanyia fujo wachezaji.

Siku ya jana mashabiki hao kama walijua kuwa timu yao itatoka na ndio maana walianza na fujo na hata kuvunja vioo vya basi la wachezaji wa Real Madrid.

Wape neno moja mashabiki wa Majogoo Liverpool.

Bofya hapa chini kutazama zaidi.

https://www.instagram.com/tv/CNrcGBtBVem/

Kama bado hujaangalia Interview ya Aristote hii hapa chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents