Habari

Silinde aingiliakati daraja Nyang’hwale (+Video)

Wananchi wa Wilaya ya Nyang’hwale katika kijiji cha Manda Mkoa wa Geita, Omary Faida Madata pamoja na mbunge wa jimbo hilo,Hussein Nassor Amar, wameiomba serikali kuwajengea daraja jipya kufuatia daraja walilokuwa waakitumia kusombwa na maji wakati wa mvua za mwezi wa kwanza na kukata mawasiliano ya vijiji viwili vya wilaya jirani ya Geita na kuanza kutumia daraja la miti ambalo wanalazimika kulipia shilingi mia mbili kuvuka.

Hayo wameyasema mbele ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, David Silinde alipofika kukagua eneo hilo nakumweleza kuwa kwasasa wanateseka sana kwa kukosekana kwa daraja hilo na kusababisha kero kulipia kuvuka kwenda upande wa pili kufuata huduma za kijamii ikiwemo afya na shule kwa kutoa shilingi mia tano ilipikipiki zao zivuke sehemu ambayo pia ni hatarishi hasa wakielekea kipindi cha msimu wa mvua.

Kwa upande wake Naibu waziri Silinde amemuagiza Meneja wa TARURA wilaya ya Nyang’hwale Benjamin Mkalava kuhakikisha ujenzi wa daraja unaanza mara moja haraka na ukamilike kabla ya msimu wa mvua kuanza kuwaondolea wananchi kero hiyo wanayoipata kwa zaidi ya miezi sita.

Aidha Naibu Waziri Silinde ameongeza kuwa, ni aibu kwa wao viongozi kwa daraja kama hilo kutojengwa kwa zaidi ya miezi yote na kumtaka meneja wa TARURA akamikishe kwa wakati na akishindwa kukamilisha kwa wakati na hawata mwelewa na atamuagiza Mtendaji mkuu wa TARURA kufika eneo hilo kusimamia.

“Mkishamaliza kujenga mniletee taarifa, mpige picha tuone watu wanapita, haiwezikani tuendelee kuiacha hivi tutakua tunamwangusha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ilani ya CCM lazima itekeleze kwa vitendo karne ya 21watu hawezi kuwa wanapita katika miti mpaka sasa hivi kwakweli mimi sikubaliano nayo” amesema Silinde

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents