Habari

Marufuku mikusanyiko isiyo ya lazima – Waziri Gwajima

Serikali imepiga marufuku mikusanyiko yote isiyo ya lazima nchi nzima, na kuagiza ile ambayo itaonekena ni lazima basi tahadhari zote dhidi ya corona zichukuliwe.

Dkt. Gwajima: Makatibu wa Afya kasimamieni nyenzo za kazi na rasilimali |  MUUNGWANA BLOG

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima amesema hatua hiyo inalenga kukabiliana wimbi la tatu la maambukizi ya virusi vya corona, ambalo madhara yake yanaendelea kujitokeza.

Katika taarifa hiyo, Waziri Gwajima amewataka Viongozi wa Serikali na wale wa sekta binafsi kuonesha mfano wa namna wanavyochukua hatua kukabiliana na ugonjwa wa corona.

Kwa mujibu wa Dkt. Gwajima, idadi ya wagonjwa wa corona imezidi kuongezeka nchini, na hadi kufikia tarehe 21 mwezi huu kulikuwa na wagonjwa 682 wanaopatiwa matibabu kwenye vituo mbalimbali vya kutolea huduma.

Pia amewataka Wananchi wote kujiandaa kupata huduma ya chanjo dhidi ya corona, ambayo itatoewa bure na kwa hiari.

Amesema jana Julai 22 Wataalamu wa afya wamekutana kupata mafunzo, tayari kwa ajili ya kuwezesha upatikanaji wa huduma ya chanjo dhidi ya corona, na kwamba taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents