HabariMichezo

Simba ya Benchikha tutarajie pira biriani.?

Hakuna asiyefahamu kuwa Mjini ameshuka Kocha wa kazi kweli, huyu ni ‘show show’ ukibisha kawaulize #Yanga kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho

Simba tunaweza kusema hapa wamelamba karata dume

Licha ya ubora wa Kocha Benchikha na benchi lake la Ufundi lakini kama hatakuwa na Mazingira rafiki, Ushirikiano kutoka kwa mabosi zake na Wachezaji basi itakuwa kazi bure hata angeshuka Pep Guardiola.

Ni wakati sasa wa @simbasctanzania kumaliza tofauti zao kuanzia Mashabiki, Wachezaji mpaka Uongozi ili kumrahisishia kazi ‘Kocha la Boli’.

Profile ya Kocha ni kubwa mno jambo ambalo haikuwa rahisi kwa watu kuamini kuwa Benchikha angekuja kuifundisha @simbasctanzania ila imewezekana.

Je, #SimbaSC ya Benchikha unaitabiria kitu gani.?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents