Habari

Sina tatizo na chama chochote – Spika Ndugai

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema kuwa hana tatizo na chama chochote kile cha siasa lakini linapofika jambo lolote mwenye kumbukumbu ya vyama vya siasa na katiba za vyama vya siasa na viongozi halali ni msajili wa vyama vya siasa na sio mtu mwingine.

Spika Ndugai ameyasema hayo alipokutana na waandishi wa habari ofisi za Bunge jijini Dar es salaam na kuzungumzia masuala kadha yanayohusu shughuli za bunge hilo.

“Sina tatizo na Chama chochote kile cha siasa, lakini linapofika jambo lolote la utaratibu ni jambo la utaratibu mwenye kumbukumbu ya vyama vya siasa na katiba za vyama vya siasa na viongozi halali ni msajili wa vyama vya siasa na sio mtu mwingine yoyote, kwahiyo linapotokea jambo linatoka na mvutano kazi yangu ni kumuuliza huyo ambaye ni muweka hazina wa vyama vya siasa kwa maana hiyo ambayo nimeieleza ambaye ni msajili wa vyama vya siasa, kwa maana ukisema humu anasema simfahamu basi na mimi nakuwa simfahamu akisema namfaham basi na mimi namfahamu lazima twende kwa utaratibu,” alisema Spika Ndugai.

Hata hivyo Spika Ndugai alisema kuwa Bunge likianza tu, wabunge wa CUF wataapishwa “Shughuli ya kwanza ya bunge mbunge akishateuliwa ni kumuapisha, sasa kwa kuwa hawa nao wamepatikana tume ya uchaguzi imeshatuletea kwa mujibu wa kanuni zetu unless kuwe na katazo la Mahakama, shughuli yetu kabisa ya tarehe 5 asubuhi ni kiapo kwahiyo wakishaapishwa mambo ya posho yanaendelea kama kawaida kama anastahili zake Mbunge anaendelea kama kawaida.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents