Habari

Mikoa ya Dar, Mwanza yaongoza kwa uhalifu mitandaoni

Ingawaje kuna sheria ya makosa ya mtandao lugha za matusi zimeendelea kutumika nchini Tanzania huku mkoa wa Dar es Salaam ukiwa kinara.

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini , (ACP) Barnabas Mwakalukwa.

Takwimu zilizotolewa jana na jeshi la polisi kupitia kwa msemaji mkuu wa jeshi hilo ACP Barnaba Mwakalukwa zimeonyesha kuwa jumla ya matukio 327 ya matusi mtandaoni yameripotiwa kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu.

ACP Mwakalukwa amesema matukio mengi ya makosa ya matusi yametokea wilaya ya Temeke huku takwimu hizo zikionyesha kupungua katika wilaya ya Kinondoni ambayo mwaka jana matukio kama hayo 911 yaliripotiwa kwenye wilaya hiyo.

Pia Mkoa wa Mwanza nao umebainika kuwa kinara kwa upande wa makosa ya wizi wa fedha mitandaoni ukilinganisha na mikoa mingine nchini Tanzania.

“Jumla ya matukio 1663 ya wizi wa fedha kwa njia ya mtandao zimeripotiwa huku mkoa wa Mwanza ukionekana kuwa kinara ikifuatiwa na Ilala na Kinondoni, Unaweza kuuliza kwa nini Mwanza, ule mji umekua kuna wafanyabiashara wakubwa, wahalifu nao wanabuni mbinu mpya,” amesema ACP Mwakalukwa.

Hata hivyo tayari jumla ya watuhumiwa 315 wamekamatwa kuhusiana na makosa ya uhalifu mtandaoni na kesi 153 zimefikishwa mahakamani na kati ya kesi hizo wahusika katika kesi 19 walikutwa na hatia na nyingine zipo chini ya upelelezi.

Kwa upande mwingine Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Hamza Hassan amesema ipo haja ya kuendelewa kutolewa elimu kuhusu sheria ya mtandao ili kupunguza vitendo vya ukiukwaji maadili.

Chanzo:Mwananchi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents