Habari

Sio muda mrefu litatoka tamko – Waziri wa fedha Dk Mwigulu Nchemba kuhusu Tozo ya miamala ya simu

Waziri wa fedha Dk Mwigulu Nchemba amezungumza na waandishi wa habari akitoa ufafanuzi kuhusiana na tozo katika miamala ya simu.

”Pande zote mbili kwa maana ya serikali na ninyi watoa huduma, hivi kweli na ninyi hizi namba hamuoni huu mzigo mzito unaosemwa sio tu shilingi 10 ya serikali, hivi kweli huku na ninyi hamuwezi mkaangalia.” – Waziri wa Fedha na Mipango nchini Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba

”Kwa hiyo hivi tunavyoongea tunamalizia malizia kuona namba ya mwisho itakuwa ipi maana na wenzetu nao tuliwapa jukumu nao  watafakari kwenye eneo hilo.” -Waziri wa Fedha na Mipango nchini Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba

”Kwa sababu kama nilivyosema nchi ni yetu, fedha ni zetu, na uwamuzi ni wetu sisi wenyewe watanzania, kwa hiyo ni namna ya kucheza na namba ili tuje na njia ambayo itakuwa mahususi, itakayokuwa muafaka, ambayo haitahathiri shughuli zetu sisi huku tunazofanya za kujiletea maendeleo.”- Waziri wa Fedha na Mipango nchini Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba

”Kwa hiyo hivi tunavyoongea, leo hii nikimaliza hiki kikao nitakuwa na kikao kingine ambacho kinahusisha kukamilisha hizo namba baada ya kuwa zimeshatoka kutoka timu ya wataalamu, na tumesha ‘network’ na Mh Waziri Mkuu atapanga kikao haraka cha kupokea hiyo taarifa.”- Waziri wa Fedha na Mipango nchini Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba

”Sio muda mrefu litatoka tamko la mwisho kitu gani ambacho kitakuwa kimeshakamilishwa na timu hizi zote za kwetu pamoja na wentu, kwakuwa watanzania wameweza kuvumilia siku hizi zote na kuendelea kuunga mkono serikali, hizi siku si nyingi waendelee kuvumilia hivyo hivyo tutatoa tamko ambalo lina husiana na ‘frame work’ ipi ambayo inakuwa nzuri zaidi inayohusisha namba ambazo zimeandaliwa upande wetu sisi lakini na upande wa kwawenzetu.”- Waziri wa Fedha na Mipango nchini Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents