Muziki

TID apongeza serikali kukusanya tsh bilioni 48 kupitia tozo za simu

 

Msanii wa muziki @tidmusic baada ya Wizara ya Fedha kutangaza kukusanya bilioni 48 kupitia tozo za simu, ameibuka na kuipongeza wizara kwa kazi nzuri.

Mkongwe huyo kwenye muziki ameenda mbali zaidi kwa kuwaelewesha watu ambao amekuwa na maoni tofauti juu ya tozo hizo.

Mapema leo Waziri Nchemba mbele ya waandishi wa habari alitoa taarifa hii “Tangu makato ya tozo yaanze kwa hizi Wiki 4 hadi leo tumekusanya zaidi ya Bilioni 48, zaidi ya Bil 22 tulishapeleka kwenye maeneo ambayo hayana vituo vya afya (zaidi ya vituo 90), leo tumepeleka zaidi ya Bil 15 kwenye eneo hilohilo na kufanya vituo kuwa zaidi ya 150“

“Kati ya hizi zaidi ya Tsh.Bil 48 tulizokusanya kwenye makato ya tozo kwa hizi Wiki nne, zaidi ya Bil 7 zimepelekwa kwenye madarasa, mtaona wenyewe tumepeleka fedha zijenge vituo 150 ambavyo vinaokoa maisha yetu, pia madarasa zaidi ya 500, ni Watoto wetu wanasoma”

“Ndani ya Wiki hizo nne za makato kwenye miamala kwa miezi hii minne kwa upande wa Zanzibar wamekusanya Bilion 1.6, kwahiyo utaona jambo hili lina matokeo” Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba, Dar es salaam leo

Written and edited by @yasiningitu

Related Articles

Back to top button