Burudani

Sitaki kufanya kolabo na mastaa, bora niwasaidie wasanii wachanga – Jaffarai

Msanii mkongwe wa muziki, Jaffarai, amesema kuwa hataki kufanya kolabo na mastaa bali atakuwa anafanya kolabo na wasanii wachanga ili kuibua vipaji vipya.
Jaffarai

Rapa huyo ambaye yupo mbioni kuachia wimbo mpya hivi karibuni, ameiambia Bongo5 kuwa alikuwa kimya ili kupisha shughuli za fiesta ambazo zinaendelea.

“Kuna kazi mpya inakuja, ni kolabo na msanii na mchanga kabisa, mimi sitaki kufanya kolabo na mastaa,” alisema Jaffarai.

Aliongeza,”Mimi ni msanii mkongwe, kuna namna nyingi ya kuwasaidia wasanii wachanga kwa kufanya nao kolabo, kwa hiyo mimi nasema mashabiki wakae mkao wa kula kwa ajili ya kazi mpya,”

Wimbo wa mwisho kuachia rapa huyo ulikuwa ni ‘Wakati’ ambao alimshirikisha Kassim Mganga.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents