Burudani

Snura asema baada ya Ramadhan ni video mpya na filamu ‘Siku 5’

Snura amedai kuwa baada ya mwezi wa Ramadhan atatoa video ya wimbo wake uliovuja ‘Unajidabua’ pamoja na filamu mpya iitwao Siku 5.

SNURAAAA

Muimbaji huyo amesema wimbo huo haujapata promotion kubwa kwakuwa ulivuja tu.

“Kiukweli wimbo haujafika mbali kwakuwa hata kuitoa rasmi sijautoa,” amesema. “Kwahiyo siwezi kuuzungumzia. Lakini sasa hivi nimeufanyia video ndo nitautoa rasmi baada ya Ramadhan.”

Kuhusu filamu ya ‘Siku 5’, Snura amesema ameshirikiana kuandika mkasa wake na Kala Jeremiah.

“Kwenye filamu nimejipanga na kazi inaitwa Siku 5. Ipo tofauti kabisa, ni hatari hiyo movie. Hii movie story nimetunga mimi na Kala Jeremiah. Kwahiyo huenda kwenye hii filamu mtamuona pia Kala, yote yanawezekana. Pia kuna filamu nyingine inaitwa Kiboko Yao, zote ni kazi ambazo zinakuja.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents