Siasa

Songwe: Akamatwa na TAKUKURU akigawa rushwa ya vitenge na fedha taslimu achaguliwe Ubunge viti maalumu

Takukuru Mkoa wa Songwe inamshikilia Mjumbe wa Baraza la UWT Taifa toka Mkoani Songwe Neema Ndabila kwa kukutwa akigawa Rushwa kwa wajumbe wa UWT wa Wilaya ya Songwe kwa lengo la kumuunga mkono ili aweze kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Viti maalumu.

Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Songwe DAMAS SUTA amethibitisha tukio hilo na amesema kuwa Neema Ndabila ni mkazi wa Tunduma na amepita katika Kata mbalimbali za Wilaya za Mbozi na Songwe ambapo wao Takukuru walimuwekea mtego ambapo wamefanikiwa kumkamata Wilayani Songwe akiwa na baadhi ya wajumbe na amekutwa na doti za vitenge pamoja na fedha taslimu.

Amesema kuwa Neema Ndabila yupo mahabusu na atakaa mahabusu mpaka Takukuru watakapokamilisha upelelezi wao na watamfikisha mahakamani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents