Habari

Sugu Atema Cheche Bungeni

Mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Joseph Mbilinyi, leo mchana amesema Mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Nne ya Rais Jakaya Kikwete wanaotamba kuwa hawatang’oka kwenye wadhifa huo, watang’olewa kwa kimbunga kinachokuja.

Akizungunza Mjini Dodoma mchana leo, amemhakikishia Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda kuwa moto uliowashwa kufuatia mawaziri waliotajwa kuhusika katika kashifa ya ubadhirifu, watang’oka.

Amesema hata kama kimbunga hicho hakitang’oa nyumba nzima,lakini kitaondoka japo paa la nyumba hiyo, akimwaanisha kuwa iwapo mawaziri hao wataendelea kung’ang’ania nyadhifa hizo, Waziri Mkuu Pinda atang’olewa kwa upepo huo.

“Sitanii, huu ni upepo wa kimbunga, kama hautang’oa nyumba, utaondoka na paa la nyumba, inasemekana kuna tetesi kuwa wameambia huu ni upepo tu utapita, ninakuhakikishia Mheshimiwa Spika, upepo huu wa kimbunga lazima utawang’oa, watake wasitake”, amesisitiza Mbilinyi.

Amewataka mawaziri walioshindwa kazi ya kuwajibika waachie ngazi, kama walivyoombwa na Mbunge wa Vunjo, Bw. Agustine Mrema wa TLP.

Mrema aliwaambia mawaziri hao kuwa iwapo kazi ya kuwajibika imewashinda, ni bora wakae kando ili wengine wafanye kazi hiyo. Huku Waziri Mkuu Pinda akionesha kutabasamu.

Aidha Sugu alisema kazi yao kama vyama vya upinzani Bungeni ni kupambana na Chama Tawala, ili kujisahihisha kwa wananchi, huku akiwataka wafanye maandalizi ya kushindana na CHADEMA watakapokuwa wapinzani.

“Mheshimiwa Spika, kazi ya kambi ya upinzania Bungeni ni kukosoa kila uozo unaofanywa na Chama Tawala, waache kufanya madudu, hii itawasaidia watakapokuwa wapinzani nao wajipange kutukosoa tutakapoingia madarakani kuwatumikia watanzania”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents