Habari

Taharuki yaibuka Kagera baada ya kufuka moshi uliodhaniwa volcano

Wananchi wa bonde la Katarabuga mkoani Kagera, wamepatwa na taharuki baada ya kuibuka moto ardhini wakidhani volcano. Hata hivyo, wakala wa Jiolojia, Prof Abdulkarim Mruma aliwatoa hofu wananchi hao kuwa ni moshi wa kawaida.

mkoa-wa-kagera

“Huu moto unaunguza ardhi ambayo umejaa vipande vipande vya miti mikavu majani, mizizi mithili ya mtu anayetengeneza mkaa,huo moto unaoungua hivi ndio unaona hili bonde,limekamatana likawa gumu kwasababu ya hiyo mizizi,kwahiyo hiyo mizizi ikishaungua hilo bonde la udongo linaachana,” alisema Mruma.

“Volcano haiwezekani hapa, volcano ni uji wa miamba na ya chini kabisa ya volcano degree 400 kwa hiyo degree 400 sentigrade ikiungua hapa hata huu mti usingesalia, volcano mara nyingi inatoka na majimaji na mvuke,” aliongeza.

“Huu ni moto wa kawaida, moto kama huu unatokea kwenye ardhi ambayo ina uozo wa majani mengi. Sasa yale majani yakiungua yanatoa kitu kama hiki. Moto wa namna hii mara nyingi unatokea kwenye makaa ya mawe mtu anapita anaangusha moto mkaa unalipuka panaanza kuungua na ardhi inachubukachubuka hivi,” alifafanua.

Tukio hilo limekuja ikiwa ni wiki kadhaa baada ya mkoa huo kukubwa na tetemeko la ardhi lililosababisha maafa makubwa.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents