Habari

Tannesco wataja mikoa itakayokosa Umeme

Kupitia mtandao wao wa Instagram wameandika kuwa:- MATENGENEZO NJIA YA USAFIRISHAJI UMEME KIDATU-IRINGA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawafahamisha wateja wake kuwa, Jumatatu Novemba 15, 2021 kutakuwa na matengenezo ya njia ya kusafirisha umeme wa kilovolti 220 kutoka Kidatu hadi Iringa kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni.

SABABU:Kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme katika gridi ya Taifa.

Kutokana na matengenezo hayo kutakuwa na upungufu wa umeme kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Mbeya, Njombe, Ruvuma, Singida, Shinyanga, Mwanza, Mara, Tabora, Arusha, Kilimanjaro na Tanga.

Tunawaomba radhi watejawetu kwa usumbufu utakaojitokeza.

Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika, toa taarifa dawati la dharura la wilaya kwa msaada zaidi au Kituo cha Miito ya Simu Makao Makuu:+255 222 194 400 na +255 768 985 100

Mitandao ya kijamii:
Twitter, www.twitter.com/tanescoyetutz,
Facebook https://www.facebook.com/tanescoyetutz

IMETOLEWA NA;
Ofisi ya Uhusiano,
TANESCO MAKAO MAKUU.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents