Habari

Surua yaibuka Afghanistan, maelfu wafariki

Shirika la Afya Duniani, WHO, linasema maelfu ya Waafghani wameathirika na mripuko wa maradhi ya surua na karibu watu 100 wamefariki dunia mwaka huu.
WHO inatahadharisha kwamba huenda watu wengi wakafariki dunia iwapo hatua za haraka hazitochukuliwa.
Shirika hilo la afya limesema mripuko huo unatia hofu kwa kuwa Afghanistan kwa sasa inakabiliwa na tatizo kubwa la usalama wa chakula na utapia mlo.
Msemaji wa WHO Margaret Harris amewaambia waandishi wa habari kwamba tangu mwanzoni mwa mwaka watu 24,000 wanashukiwa kuambukizwa ugonjwa huo na karibu visa 2,400 vya surua vimethibitishwa baada ya uchunguzi wa kimaabara.
Umoja wa Mataifa umeonya mara kwa mara kwamba Afghanistan inaelekea kukabiliwa na mzozo mbaya zaidi wa kibinadamu duniani, wakati ambapo zaidi ya nusu ya nchi hiyo inakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.
Watu wengine mamilioni pia wameamua ama kuhama au kusalia na njaa nchini humo huku msimu wa baridi ukiwa unakaribia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents