Siasa

Rwanda: Nyota wa YouTube amehukumiwa miaka saba jela kuikosoa serikali

Nyota wa YouTube wa Rwanda amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela kwa kuikosoa serikali. Dieudonné Niyonsenga, anayejulikana kama Cyuma au “Iron”, alipatikana na hatia ya kughushi, uigaji na kuwadhalilisha maafisa wa serikali.

Anakanusha madai hayo na kusema atakata rufaa. Video zake zimeshutumu askari kwa unyanyasaji mkubwa dhidi ya wakaazi wa makazi duni wakati wa marufuku ya kutoka nje katika kipindi cha janga la Corona

Mtu mwingine maarufu wa YouTube hivi majuzi alihukumiwa kifungo cha miaka 15 kwa kuchochea vurugu.

Mamlaka ya Rwanda mara kwa mara inashutumiwa kwa kukandamiza upinzani na kuwafunga jela wale wanaoikosoa serikali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents