Michezo

TANZIA: Maneno ya klabu ya Yanga, Haji Manara na Haruna Niyonzima baada ya kifo cha mzee Akilimali – Video

Maneno ya klabu ya Yanga,Haji Manara na Haruna Niyonzima baada ya kifo cha Akilimali - Video

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Klabu ya Yanga Sc mzee Ibrahim Akilimali amefariki dunia, leo alfajiri wilayani Bagamoyo mkoani Pwani. Tutaendelea kukuletea taarifa kamili kuhusu msiba huu.

Maneno ya Haji Manara baada ya kifo cha Akilimali.

“Tumeondokewa, Mwamba katika Miamba ya kabumbu Nchini umeanguka,Mzee wetu,Baba na Babu yetu, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Yanga Ibrahim Akilimali katangulia mbele ya haki, poleni Familia, poleni Wanayanga,huu ni msiba wetu sote na tutashiriki kikamilifu kwenye majonzi haya”

https://www.instagram.com/p/B6CkBCrBMer/

Maneno ya klabu ya Yanga baada ya kifo cha Akilimali.

Tanzia:
Klabu ya Yanga inasikitika kutangaza kifo cha Mwanachama wetu Maarufu na Mzee wetu Ibrahim Akilimali kilichotokea alfajiri ya leo Bagamoyo Mkoani Pwani. Maziko yanatarajiwa kufanyika kesho saa 10 jioni Tandale kwa Mtogole.
Innah lillah wainnah ilayh rajiuun.. Haikuwa Dunia ila ni mapito.

https://www.instagram.com/p/B6CokfNAbSh/

Maneno ya Haruna niyonzima.

https://www.instagram.com/p/B6C4lNElHzl/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents