Habari

TB Joshua alitabiri mauaji ya Colorado


Mhubiri maarufu wa nchini Nigeria, TB Joshua ambaye hujiita Nabii, alitabiri mauaji ya ijumaa iliyopita kwenye jumba la sinema huko Denver, Colorado nchini Marekani ambapo watu 12 waliuawa na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa.
Mtu aliyetekeleza mauaji hayo anaitwa James Holmes aliyeingia na silaha nzito kwenye jumba hilo la sinema lililokuwa likionesha filamu mpya ya Batman.
Wakati habari hiyo ikiwa bado inaandikwa katika angle mpya kila kukicha, kumetolewa video kwenye mtandao wa YouTube ambapo mhubiri huyo alitabiri tukio hilo.
Katika video hiyo iliyorekodiwa tarehe 10 June mwaka huu, Joshua anasema “Katika taifa la Marekani, wanapaswa kusali. Namuona mwanaume amebeba bunduki kwenye umati wa watu na kuanza kushoot. Watu wengi watauawa kabla hajakamatwa.
Utabiri huo ulioneshwa live kwenye kituo cha TV cha Emmanuel TV.
T.B. Joshua ni mhubiri maarufu sana barabi Afrika, alikuwa rafiki wa karibu wa rais wa Ghana aliyefariki jana John Atta Mills, rais wa Malawi Joyce Banda na waziri mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangarai.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents