Habari

Tanzania kufanya kampeni ya utalii kwenye mashindaano ya Olimpiki



Mwezi ujao Tanzania itaanzisha kampeni mahsusi ya kutangaza utalii inayoilenga Uingereza na maelfu ya watu wanaohudhuria michuano ya Olimpiki jijini London.
Katika kampeni hiyo yatabandikwa matangazo kwenye magari makubwa nchini Uingereza kuinadi sekta hiyo nchini humo katika msimu huu wa mashindano hayo ya Olimpiki.
Mpango huo utahusisha zaidi ya magari kumi yakiwemo magari makubwa, Range Rover na Land Rover ambazo zitakuwa zimebandikwa vivutio vya utalii nchini Tanzania vikiwemo Mlima Kilimanjaro, Mbuga ya wanyama ya Serengeti, Mikumi, Selous na vivutio vingine.
Kampeni hiyo itafanywa na kampuni ya Uingereza inayomilikiwa na watanzania ya Serengeti Freight Forwarders.
Imesema imeamua kufanya hivyo kama ishara ya uzalendo kwa nchi yao na inaaamini itapenya nchini Uingereza pamoja na masoko ya Ulaya.
Mkurugenzi mtendaji wa Serengeti Freight Forwaders Chris Lukosi ameliambia gazeti la ‘Daily News’ kuwa tayari wamepata fedha za kununua gari hizo na zitasambazwa katika barabara za miji ya London, Manchester na Birmingham.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents