Habari

TCAA: FastJet walipe deni la tsh bilioni 6 na watupe andiko kuthibitisha uwezo wao wa kifedha

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Fadhili Manongi, amesema FastJet hawana ndege hata moja hivyo kama mamlaka ya TCAA hatuna budi kuwazuia na wana madeni ya 6 billion hivyo kama wao wanahitaji kufanya biashara wafuate masharti na walipe madeni

Pia alisema tunawataka walete andiko la kudhibitisha uwezo wa kufedha ili kuona kama wanajiweza, Kwa mujibu wa sheria lazima ulipe madeni yako yote ili uweze kuendelea na biashara.

Tarehe 24/12 saa 6 mchana wameleta maombi ya kuleta ndege zenye usajili wa Afrika Kusini ndiyo zimeletwa halafu tarehe hiyo hiyo wameleta maombi na barua ya Mkurugenzi mtendaji kumteua Lawarence Masha kuwa accountable manager

Ndege aina ya Embraer 190 iliyokodiwa baada ya Fastjet kufungiwa haitaruhusiwa kuondoka nchini mpaka Fastjet walipe madeni wanayodaiwa.


Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents