Habari

RC Makonda awataka viongozi wa dini kuacha kupokea sadaka za mafisadi na wala rushwa (Video)

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewakutanisha Viongozi wa Dini wa madhehebu yote na kupata nao chakula cha pamoja ikiwa ni sehemu ya kuthamini kazi nzuri na kubwa inayofanywa na viongozi wa Dini katika jamii.

RC Makonda amesema Viongozi wa Dini wamekuwa chachu kubwa katika kudumisha Amani, umoja na mshikamano katika jamii jambo linalopelekea ustawi Bora wa Taifa.

Aidha RC Makonda amesema anachokiamini ni kwamba Kama kila mwananchi atakuwa na hofu ya Mungu ndani ya jamii hakutakuwa na matukio ya Ujambazi, wizi, uporaji, mmomonyoka wa maadili, uhasherati, ushoga, matumizi ya dawa za kulevya hivyo amewasihi viongozi wa dini kusimama kidete na kutumia madhabau kuwahubiria wananchi.

Pamoja na hayo RC Makonda amewaomba viongozi wa Dini kuliombea taifa na viongozi wake huku akielezea kazi kubwa na nzuri inayofanya na Uongozi wa Rais Magufuli.

Kwa upande wa viongozi wa dini walioshiriki hafla hiyo wakuwemo maaskofu, wachungaji, mitume,mapadri, manabii na masista kwanza wameshururu kukutanishwa pamoja ambapo wamemuelezea RC Makonda Kama kiongozi mwenye hofu ya Mungu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents