Burudani

Tumerejea toka mapumzikoni Mombasa

team_b5

Ni siku tano tangu timu ya bongo5 ichomoke kwenda mapumziko ya kikazi katika miji miwili ya pwani. Moja kati ya mji huo ni kisiwa cha Mombasa,Kenya, maarufu sana kwa utalii na historia na Tanga ambao nao ni mji kando ya bahari ya hindi nchini Tanzania.

Bongo5 ilifanikiwa kuonana na TID, Nameless na Wahu ambao wote walikuwa kisiwani hapo kwa mualiko wa kufanya shoo iliyokwenda kwa jina la ‘Niaje X Mass Beach Party. Ndani ya viwanja vya hoteli ya pwani Big Tree iliyopo eneo la Nyali jijini.

tid

Party hiyo ambayo ilikuwa chini ya uratibu wa niaje.com ilifanyika usiku wa kuamkia sikukuu ya xmass ilianza mida ya saa tano usiku na kuendelea hadi majira ya saa nane na robo usiku.

Bongo5 ilibahatika kukutana na promota maarufu wa kike mjini humo bibie Eve ambaye aliongelea kwa kina mzozo wake na msanii Chege ambapo utamsikia kupitia upande wetu wa video akiongelea mkasa mzima na msanii huyo kutoka pande za Temeke.

Tulitembelea eneo maarufu la kihistoria jijini Mombasa, Fort Jesus ambapo historia ya uongozi , mamlaka za kikoloni na ustawi wa jiji hilo inapatikana sawia.

FJ

Baada ya kuondoka kumaliza vya Mombasa, Bongo5 ilihamia jijini Tanga ambako tulikutana na Fid Q, Salama J pamoja na Musa Hussein na Daniel Nyalusi ambao wote kwa njia moja ama nyingine ni wadau wa mambo ya habari, burudani ya muziki na filamu.

fort-2

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents