Burudani

TEEN EXTRA AWARD BADO KITENDAWILI?!

Katika hali ya kusikitisha teen extra award zimezimika kama mshumaa kweye upepo. Teen extra award hizi ni tuzo zilizokuwa zimeandaliwa na timu nzima ya XXL kipindi maarufu kwa burudani Tanzania kinachorushwa na redio ya watu a.k.a Clouds FM, award hizi zilisikika na zilitangazwa kwa mbwembwe za kutosha kabisa mpaka kufikia hata kuipa

hofu timu uandaaji wa award za kili lakini cha kushangaza mbio zote zile zimepiga mweleka na kupotelea gizani na wala hatujui mchawi ni nani pande zile kwani hata wao wenyewe (waandaaji) hatuwasikii kabisa akilizungumzia jambo hili, mimi kama mdau wa sanaa nzima ya bongo nauliza niaje ni vipi?

Nilijiuliza kuwa Dozen, Fetty na Mchomvu kweli wameshindwa gemu au wamekula za uso!? Maana kiukweli hao ndio waliokuwa mstari wa mbele katika kuliandaa na kulifanikisha suala hili mpaka ilifika hatua ya kuzindua awrd zenyewe kwa mbwembwe kali mjini hapa kwa kufanya bonge la pati (sherehe) ya uzinduzi ambao walialika mpaka wasanii kwa kuwaimbisha pale CINE CLUB na kuwachezesha watu michezo kibao tu ya bichi, lakiniiiiii nikashangaa wameingia mitini wazeiya……..

Mnajua ni nini mazee!??! Kama vipi jipangeni upya mazee msikurupuke tu na kusema mnaanzisha kitu ambacho baadae mnakuja kuonekana kama ni mbio za sakafuni bana!

Kwa maana hata kwenye kumbukumbu zangu zinanipa na akili inanituma kwa konfince za kutosha kuwa inawezekana hata ile bash mlioinzisha na kuipa jina la INTER SCHOOL BUSH ambayo kwa mara yakwanza mliifanya mwezi wa saba mwaka jana (2009) pale kunduchi nalo pia mmengukia pua! Au sio?! Maana kwa kauli yenu wenyewe mlituambia kua tamasha lile litakuwa likifanyika kila kipindi cha mwisho wa likizo za wanafunzi likini pia na hilo chali?!

Kiukweli mkianza kitu mnajua ni jinsi gani mtakitasngaza maana katika suala la matangazo naweza kusema kuwa nawapa saluti lakini ikifika katika suala la uendelezaji hapo nipo ninakuwa na kigugumizi na wala sijui niwape aslimia ngapi kwa maana naona kama mnajaribu vile!?!

Haya maswali kibao yalisumbua sana hapa bongo5 lakini baada ya kujiuliza maswali yote hayo ilibidi bongo5 imtafute mmoja wa waandaaji wa tuzo hizo ili kuzungumzia hili jambo. Bongo5 iliweza kumpata bwa Hamis Mandi a.k.a B12(B dozen) na alisema kilichowasibu mpaka tuzo hizo za teen extr kupiga mweleka.
Dozen alituweka wazi kuwa kweli wamekuwa kimya sana bila kueleza nini kitu gani kilitokea mpaka tuzo zikazimika kama mshumaa kwenye upepo. B12 mwenye manjonjo mengi wakati akiwa kwenye kipaza alisema “tuzo za Teen Extra zimezimika kwa sababu tulisimamishwa na basata kwa kile walichodai ni kuto zisajili, lakini sisi kama waandaji wa tuzo tuliona kama hakuna umuhimu wa kusajili hizi tuzo kwa sababu sisi tuzo zetu ni za muziki na masuala yote tunayofanya hapa XXL na ndio maana hata katika kategori zetu hatujaweka aina ya muziki zaidi ya bongo fleva, ila cha msingi ni kwamba tunasema tuzo hizo zipo na tutazitoa mara baada ya hili tamasha la fiesta kuisha”

Kuhusu suala la kuanzisha tuzo bila kuzisajili b12 alifafanua kwa kusema “huwa ni kawaida kwa kila tamasha kusajiliwa baada ya maandalizi yote kukamilika ili hata ukienda kusajili uwe na reference za kutosha na bajeti nzima ya tukio lenyewe”

Bwana dozen aliomba radhi kwa mashabiki kwa usumbufu wote uliojitokeza hapa kati na kuwa ahidi kuwa tuzo zipo na zitatolewa tu wala wasiwe na wasiwasi.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents