AfyaVideos

Teknolojia mpya ilivyomsaidia mtu aliyepooza kutembea (+ Video)

Mwanamume aliyepooza kufuatia kukatika kwa uti wa mgongo ameweza kutembea tena, kutokana na kipandikizi kilichotengenezwa na timu ya watafiti wa Uswizi.

Ni mara ya kwanza mtu ambaye amekatwa kabisa uti wa mgongo kuweza kutembea bila msaada.

Teknolojia hiyo hiyo imeboresha afya ya mgonjwa mwingine aliyepooza kiasi kwamba ameweza kuwa baba.

Utafiti huo umechapishwa katika jarida la Nature Medicine.

Michel Roccati alikuwa amepooza baada ya ajali ya pikipiki miaka mitano iliyopita. Uti wa mgongo wake ulikatwa kabisa na hakuwa na hisia hata kidogo katika miguu yake.

Lakini sasa anaweza kutembea kwa sababu ya upandikizaji huo ambao umeunganishwa kwa njia ya upasuaji kwenye mgongo wake.

Mtu aliyejeruhiwa kwa njia kama hii hajawahi kutembea hivi hapo awali.

Watafiti hao wanasisitiza kuwa si tiba ya jeraha la uti wa mgongo na kwamba teknolojia hiyo bado ni ngumu sana kutumiwa katika maisha ya kila siku, lakini wanaipongeza kama hatua kuu ya kuboresha maisha.

TH

Haikuwa teknolojia pekee iliyochangia Michel kupona. Muitaliano huyo anasema alipopata ajali, alikuwa na azimio la kupta maendeleo kadiri awezavyo.

“Nilikuwa nikipiga ngumi, kukimbia na kufanya mazoezi ya mwili. Lakini baada ya ajali, sikuweza kufanya mambo ambayo nilipenda kufanya, lakini sikuruhusu hisia zangu kushuka. Sikuwahi kusimamisha safari yangu ya kupona, nilitaka kutatua tatizo hili.”

Kasi ya kupona kwa Michel ilimshangaza daktari wa upasuaji wa mishipa ya fahamu ambaye aliingiza kipandikizi na kuunganisha kwa ustadi elektrodi kwenye nyuzi za neva.

Utafiti huo umeungwa mkono na Dk Ram Hariharan, mshauri katika Hospitali Kuu huko Sheffield ambaye ni huru kutoka kwa timu ya utafiti na pia anazungumza kwa niaba ya Chama kinachohusika na c majeraha ya mgongo.

“Wamefanya jambo ambalo halijafanyika hapo awali.

“Sijasikia kuhusu utafiti wowote ambapo wameweka kipandikizi kwa mgonjwa aliyekatwa kabisa uti wa mgongo kuweza kuboresha usawa, kusimama na kutembea.”

“Tunahitaji idadi zaidi ya wagonjwa ili kuonyesha kwamba ni salama kwanza na kwamba inaboresha maisha yao kwa kiasi kikubwa. Hapo ndipo inaweza kuendelezwa.”

Mishipa katika uti wa mgongo hutuma ishara kutoka kwa ubongo hadi kwa miguu. Baadhi ya watu wamepooza mishipa ya fahamu inapoharibika kutokana na kuumia.

Kwa upande wa Michel hakuna ishara kabisa kwa miguu yake kwa sababu uti wa mgongo umekatika kabisa. Lakini kipandikizi hiki hutuma ishara moja kwa moja kwa miguu yake na kumwezesha kutembea, lakini wakati tu kipandikizi kimewashwa.

Michel Walking Top

Kufikia sasa watu tisa wamepokea kipandikizi na kurejesha uwezo wa kutembea. Hakuna hata mmoja wao anayeitumia kuwasaidia kutembea katika maisha yao ya kila siku kwa sababu ni ngumu sana katika hatua hii. Badala yake, wanakitumia kufanya mazoezi ya kutembea ambayo hufanyisha misuli yao mazoezi na kuboresha afya zao.

David M’zee alikuwa mmoja wa wagonjwa wa kwanza kupokea upandikizaji huo. Kama Michel, aliweza kutembea na kipandikizi huku akitumia kifaa cha kumsaidia. Afya ya David iliimarika kiasi kwamba aliweza kupata mtoto wa kike na mpenzi wake Janine, jambo ambalo halikuwezekana baada ya ajali yake mwaka 2010.

Bado kuna safari ndefu kabla ya teknolojia hiyo kutumiwa kusaidia watu waliopooza kutembea, kulingana na Prof Grégoire Courtine, aliyeongoza timu iliyounda teknolojia hiyo katika Chuo cha École Polytechnique Fédérale de Lausanne (EPFL).

“Hii sio tiba ya jeraha la uti wa mgongo, lakini ni hatua muhimu ya kuboresha hali ya maisha ya watu. Tutawawezesha watu. Tutawapa uwezo wa kusimama na kutembea. Ni mafanikio makubwa.”

Tiba itahitaji kuzaliwa upya kwa uti wa mgongo, matibabu ambayo bado yako katika hatua ya awali ya utafiti. Prof Courtine anaamini kwamba teknolojia yake ya kupandikiza inaweza kutumika pamoja na matibabu ya kurejesha neva pindi tiba itakapokuwa tayari.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents