Michezo

Tetesi za usajili barani Ulaya Ijumaa hii, Solskjaer, Wan-Bissaka, De Gea, Hazard, Under, Sterling na wengine sokoni

Kaimu Meneja Ole Gunnar Solskjaer ndio mgombea mkuu anayepigiwa upatu kuwania kazi hiyo ya kudumu Manchester United. (ESPN). United imemtambua beki wa Crystal Palace Aaron Wan-Bissaka, mwenye umri wa miaka 21, mlinzi wa Napoli Kalidou Koulibaly, mwenye umri wa miaka 27, na mchezaji wa kiungo cha kati wa Barcelona Ivan Rakitic, aliye na umri wa miaka 30, kama wachezaji wakuu inayowalenga katika msimu wa joto (Talksport)

Watafanya uamuzi katika mwezi ujao iwapo kuanzisha majadiliano kuhusu kuongezwa muda wa mkataba wa kapteni Antonio Valencia. Mchezaji huyo raia wa Ecuador mwenye umri wa miaka 33 hajawahi kucheza tangu Januari 2. (Manchester Evening News)

Chelsea imefungua upya mazungumzo na mshambuliaji wa Ubelgiji Eden Hazard, mwenye umri wa miaka 28, huku Real Madrid ikiwa bado ina hamu ya kumsajili mchezaji huyo. (Le10 Sport)

Roma ipo radhi kumuuza winga raia wa Uturuki Cengiz Under katika jitahada za kupata fedha. Mchezaji huyo mwenye miaka 21analengwa na Arsenal. (Corriere dello Sport)

Liverpool imetuma maafisa wake Uturuki kwenda kumchunguza mchezaji mwenye umri wa miaka 19 anayeichezea kiungo cha kati Trabzonspor – Abdulkadir Omur. (Talksport)

Winga wa England Raheem Sterling, mwenye umri wa miaka 24, anasema amejihisi kuwa katika shinikizo zaidi kushinda ligi kuu England katika iliyokuwa klabu yake Liverpool kuliko katika timu aliopo Manchester City. (Sky Sports)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Lazio na Serbia Sergej Milinkovic-Savic, mwenye umri wa miaka 24, huenda akasalia Italia na akaelekea AC Milan au Inter Milan, licha ya tuhuma za Manchester United na Real Madrid kuvutiwa naye. (Goal)

Meneja wa Bristol City Lee Johnson na Bosi wa Kilmarnock, Steve Clarke ni wanaopigiwa upatu kwa kazi ya kudumu ya ukufunzi huko Fulham baada ya kutimuliwa Claudio Ranieri. (Mirror)

Mchezaji wa Tottenham na Korea kusini Son Heung-Min, mwenye umri wa miaka 26, hametajwa kama mchezaji bora katika ligi kuu ya England mwaka huu katika tuzo ya soka London huku mchezaji wa West Ham akishinda tuzo ya mchezaji kijana bora. (Standard)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents