Michezo

Tetesi za usajili barani Ulaya Jumatatu hii, De Gea hati hati PSG, Wan-Bissaka, Meunier, Silva, Sessegnon, Butland na wengine sokoni

Tetesi za usajili barani Ulaya Jumatatu hii, De Gea hati hati PSG, Wan-Bissaka, Meunier, Silva, Sessegnon, Butland na wengine sokoni

Manchester United itampa kipa wa Uhispania David de Gea £20m iwapo mchezaji huyo mwenye miaka 28 ataelekea Paris St-Germain msimu huu wa joto. (Sun)

United imekataliwa ombi lake na Crystal Palace la thamani ya £40m kumsajili mchezaji wa timu ya taifa ya England ya wachezaji wa chini ya miaka 21 Aaron Wan-Bissaka. Timu hiyo ya Eagles inataka takriban £60m. (Sky Sports)

Mkufunzi wa Arsenal Unai Emery amefanya mazungumzo na beki wa kulia wa PSG na timu ya taifa ya Ubelgiji Thomas Meunier, mwenye umri wa miaka 27, kuhusu uwezekano wa kuhama msimu huu wa joto.(Express)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Manchester City David Silva, mwenye umri wa miaka 33, atashiriki katika mechi ya mtihani uwanjani Etihad Stadium mwakani. Mkataba wa mchezaji huyo wa Uhispania unamalizika mwaka ujao na anataka asitishe kazi yake huko Las Palmas. (Sun)

Tottenham itawasilisha ombi kwa Fulham kumwania winga wa timu ya taifa ya England ya wachezaji wasiozidi miaka 21 Ryan Sessegnon, mwenye umri wa miaka 19, msimu huu wa joto. (Football.London)

Mkataba wa mchezaji huyo wa Uhispania unamalizika mwaka ujaoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMkataba wa mchezaji wa kiungo cha kati wa Manchester City David Silva unamalizika mwaka ujao

Chelsea imefufua hamu yake ya kutaka kumsajili winga wa Bayer Leverkusen na timu ya taifa ya Jamaica Leon Bailey, mwenye umri wa miaka 21, lakini ni lazima isubiri kuona iwapo marufuku iliyopewa ya uhamisho wa wachezaji itabatilishwa kabla ya kuwasilisha ombi hilo. (Mail)

Arsenal ina hamu ya kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Fiorentina Jordan Veretout, mwenye umri wa miaka 26, lakini mchezaji huyo wa zamani wa timu ya tiafa ya Ufaransa ya wachezaji wasiozidi miaka 21 tayari anafanya mazungumzo na Napoli. (L’Equipe)

Newcastle na Southampton zimewasilisha ombi kwa mshambuliaji wa Mainz na timu ya taifa ya Ufaransa ya wachezaji wasiozidi miaka 21 Jean-Philippe Mateta, aliye na miaka 21. (L’Equipe, kupitia Sport Witness)

Arsenal inataka kumsajili mlinzi wa Saint Etienne William Saliba, mwenye miaka 18, lakini timu hiyo ya Ligue 1 inataka kumchukua kwa mkopo msimu ujao wa joto. (Football.London)

Newcastle na Southampton zimewasilisha ombi kwa mshambuliaji wa Mainz na timu ya taifa ya Ufaransa ya wachezaji wasiozidi miaka 21 Jean-Philippe Mateta,Haki miliki ya pichaJEAN-PHILIPPE KSIAZEK
Image captionNewcastle na Southampton zimewasilisha ombi kwa mshambuliaji wa Mainz Jean-Philippe Mateta

Stoke inatisha £23m ili kumuuza kipa wa timu ya taifa wa England Jack Butland, mwenye umri wa miaka 26. (Sun)

Mshambuliaji wa Fulham na Serbia Aleksandar Mitrovic, mwenye umri wa miaka 24, analengwa na West Ham. (Mail)

West Ham ipo tayari kushindana na Arsenal na Tottenham kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Atalanta na timu ya taifa ya Ivory Coast Franck Kessie. Mchezaji huyo wa miaka 22 amekuwa akicheza kwa mkopo huko AC Milan tangu 2017. (Express)

Leicester itaendelea na mazungumzo na Luton Town kuhusu kumsajili beki kamili mwenye miaka 21 James Justin. (Mail)

Aliyekuwa kipa wa Manchester United Anders Lindegaard anasema David Moyes kupewa fursa kumpokea Sir Alex Ferguson huko Old Trafford ni kama “kuchaji simu ya iPhone kwa chaja ya Nokia “. (Standard)

Leeds imewasilisha maombi kwa Liverpool kuonyesha hamu ya kutaka kawasajili winga Harry Wilson na Ryan Kent, wote wenye miaka 22. (Football Insider)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents