Habari

The Chase: Nando adai alilazimishwa na Selly kufanya mapenzi ‘peku’ na kumwambukiza gonjwa la ngono

Mmoja wa wawakilishi wa Ghana kwenye msimu wa 8 wa Big Brother Africa, Selly aliyaaga mashindano hayo siku kadhaa baada ya mwakilishi wa Tanzania, Ammy Nando kumshutumu kuwa amemuambukiza ugonjwa wa ngono (STD) pindi wawili hao walipoamua kujamiiana ndani ya jumba hilo.

546624_324919007586612_369082865_n

Nando ameendelea kuchukizwa na ukweli kuwa ameambukizwa gonjwa hilo na amekuwa akiwaeleza washiriki wenzake bila kuficha.

“Unajua namchukia sana mal**ya huyo. Nimechanganyiwa sababu mal**ya huyo amenipa STD. Ndio maana jana blood pressure ilikuwa juu sana,” alimwambia Methiopia Bimp.

Kwa mujibu wa Nando, alitaka kutumia condom kabla ya kufanya mapenzi na Selly, lakini msichana huyo alikataa na kudai alitaka wafanye pekupeku na Nando kujikuta akikubali bila kujua angeambukizwa.

EvictedProfile_0020_74d1aab9-1a24-4e1d-bbad-f477f8add475_571314205712711

Ripoti zinadai kuwa madaktari wanaendelea kumtibu Nando ugonjwa huo wa Chlamydiae. Hata hivyo hakuna ushahidi kuwa Nando aliupata kwa Selly.

Mapenzi hayo kati ya Selly na Nando yalikuwa habari kubwa nchini Ghana kwasababu msichana anafahamika kuwa na uhusiano na Steven Fiawoo aka Praye Tiatia.

Mama yake Selly, Benedicta Galley amekiambia kipindi cha Entertainment Review cha Peace FM ya nchini Ghana kuwa huenda Nando alitumia ‘juju’ kwa binti yake kwakuwa amemlea kwenye maadili mazuri na amekuwa na uhusiano na Praye Tiatia kwa zaidi ya miaka minne.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents