Burudani

TPF6 Academy Day 4: Hisia apewa surprise kwenye birthday yake, apewa busu zito na Angel

Leo ni siku ya 4 tangu washiriki wa shindano la Tusker Project Fame msimu wa 6 waingie kwenye academy. Soma yaliyojiri leo.

tpf6

Somo la Dance la Mwalimu Edu

Washiriki walianza kwa somo la dance kutoka kwa mwalimu Edu aliyewafundisha mitindo mbalimbali ya kucheza na kuwakumbusha umuhimu wa kuwa na mawazo chanya katika kufanikisha kushika somo hilo.

Washiriki wajadili performance za Jumapili

Baadaye washiriki walikaa pamoja na mwalimu wa Kavutha kuangalia video za baadhi ya performance za Jumapili iliyopita huku washiriki wengine wakitoa ushauri kwa baadhi ya makosa waliyogundua. Baadhi ya performance zilizooneshwa zilikuwa ni za Nyambura wa Kenya na The Undercover Brothers wa Uganda. Angel wa Tanzania na Mwalimu Kavutha aliwashauri jamaa hao wa Uganda kuimba kama kitu kimoja na kuepuka kupisha kwa sauti zao.

Hisia afanyiwa surprise kwenye birthday yake

Mwakilishi wa Tanzania, Hisia alifanyiwa surprise ya nguvu kutoka kwa washiriki wenzake pamoja na muimbaji Erick Wainaina ambaye ni miongoni mwa walimu wa faculty. Erick alikuwa amebeba keki iliyokuwa imeandikwa jina la Hisia huku akiwaongoza washiriki wengine kumuimbia wimbo wa birthday Hisia. Angel, alimfuata Hisia na kumpa kumbatio la uhakika na kumbusu mshiriki mwenzie kutoka Tanzania na baadaye Hisia kuizungumzia busu hiyo.

Washiriki wapewa namba za ushiriki

Leo washiriki hao wamepewa namba za ushiriki zitakazotumika katika mchakato wa kuwapigia kura.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents