Habari

TRA yayataka makanisa kutochanganya sadaka na mapato mengine

Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imewataka maparoko na viongozi wengine, kutochanganya sadaka na mapato mengine wakati wakiandaa mahesabu yao kwani hiyo inaweza kusababisha watozwe kodi kubwa ya mapato isiyostahili.

Hayo yalisemwa Jumanne hii na Meneja wa Elimu ya mlipa kodi ya mamlaka hiyo, Diana Masala alipokuwa akizungumza kwenye semina ya viongozi kanisa la jimbo kuu la kanisa Katholiki jimbo kuu la Dar es Salaam.

“Kwakuwa sadaka na zaka huwa hazitozwi kodi, wakati wa kuandaa sadaka zenu na mapato ya kanisa lazima myatenganishe ili yajulikane sadaka ni ipi na mapato mengine ni yapi. Kuyajumisha mapato hayo bila kuyachanganua mtatozwa kodi kubwa kinyume na kanuni za TRA,” alisema Masala.

Aidha Masala alisema hesabu hizo zinatakiwa kuwa na tofauti hata kwenye benki.

BY: EMMY MWAIPOPO

CHANZO: MWANANCHI

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents