HabariPicha

Treni yaanza safari zake

Abiria wakipanda moja ya mabehewa ya treni. (Photo from haki-hakingowi)Imechukua takribani mwaka mmoja tangu safari za Treni kusimamishwa jijini Dar es Salaam, hatimaye Serikali kupitia Kampuni ya Reli (TRL), imewezesha kukamilisha uanzishaji wa huduma za usafiri huo kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza na Kigoma.

Abiria wakipanda moja ya mabehewa ya treni. (Photo from haki-hakingowi)

 

Imechukua takribani mwaka mmoja tangu safari za Treni kusimamishwa jijini Dar es Salaam, hatimaye Serikali kupitia Kampuni ya Reli (TRL), imewezesha kukamilisha uanzishaji wa huduma za usafiri huo kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza na Kigoma.

 

Wakati zilipokuwa zimesimamishwa safari za treni za kuanzia hapa jijini zilikuwa zikiendelea na safari zake kwa kuanzia Dodoma.

 

Novemba mosi Treni iliondoka saa 11 jioni na kuanza safari zake kwani kutokana na kusimama kwake kulikuwa na malalamiko kwa baadhi ya wakazi kulalamikia kutumia gharama kubwa miezi kadhaa iliyopita ambako wamekuwa wakilazimika kupanda mabasi kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kwa ajili ya kwenda kuifuata treni.

 

Mkurugenzi Msaidizi wa Usafiri wa Nchi Kavu kutoka Wizara ya Miundombinu, Benard Liamba, alisema hali hiyo imesababishwa na matunda mazuri yaliyosababishwa na Kampuni ya TRL iliyokodishiwa muda mfupi na lililokuwa Shirika la Reli Tanzania (TRC).

 

Liamba alisema mkataba kati ya Serikali na TRL unaelekeza kampuni hiyo kutoka India, kutoa huduma mara sita kwa wiki na treni nne kutoka Dar es Salaam kwenda Bara.

 

Waziri alisema kutokana na uchache wa vichwa na mabehewa, itafanyika safari moja kwa wiki hadi itakapofika Novemba 18 mwaka huu, watakapoongezwa. Huduma ya usafiri wa treni ya kati kutoka Dar es Salaam ilisimamishwa Aprili mwaka jana, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni uhaba wa mabehewa uliosababishwa na kuchakaa na ubovu wa reli katika baadhi ya maeneo kati ya Dodoma na Dar es Salaam.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents