Habari

Jukwaa la Wazi kwa umma kujadili Afya za akina mama

MASHIRIKA 10 ya wanaharakati za kutetea wanawake pamoja na haki za binadamu, yameandaa Jukwaa la Wazi kwa Umma kujadili mambo yanayoathiri afya za wasichana na wanawake hapa nchini.

MASHIRIKA 10 ya wanaharakati za kutetea wanawake pamoja na haki za binadamu, yameandaa Jukwaa la Wazi kwa Umma kujadili mambo yanayoathiri afya za wasichana na wanawake hapa nchini.


Masuala yatakayojadiliwa ni pamoja na vifo vya wazazi, wajawazito, watoto, vipigo ukatili dhidi ya wanawake na wasichana walioajiriwa kufanya kazi majumbani. Jukwaa hilo la wazi la siku tatu linaanza Jumatatu ijayo katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Utu Mwanamke linalojishughulisha na masuala ya ustawi wa wanawake, Maggie Bangser, alisema jijini katika mkutano wa waandishi wa habari na kuongeza kuwa washiriki katika jukwaa hilo ni wabunge, polisi, wanataaluma, wanasheria, madaktari, wanahabari, wanaharakati wa haki za binadamu na umma na kwamba hakutakuwa na kiingilio.


Bongser alisema lengo kubwa la mjadala huo ni kuiwezesha umma kujadili jinsi ya kupunguza matatizo hayo.


Alisema kuwa watakuwa na baadhi ya wanawake ambao wamewahi kuteswa kwa kupigwa na waume zao, wafanyakazi wa majumbani waliofanyiwa ukatili na waajiri wao watakuwa ni miongoni mwa watakaohuduhuria na kutoa ushuhuda wao hadharani.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents