Burudani

Tuerny afunguka suala la kusema hajatulia “Sikumbuki mara ya mwisho kupika”

Mrembo Tuerny ambaye kwa sasa anatikisa mitandao na kuwatoa udenda wanaume wengi kutokana na urembo wake amefunguka mambo kadhaa usiyoyajua kuhusu maisha yake pamoja na safari yake mpya ya muziki.

Msanii huyo wiki hii alikuwa kwenye Cook with Wema Sepetu ambapo alifunguka vitu mbalimbali, moja aliulizwa mara yake ya mwisho kupika.

“Nimepikaa, si kukumbuki,” alisema Tueny. Alipoulizwa kama ana anapikaga nyumbani au kumpikia shemeji alisema “Sipikagi, labda nianze kumpikia,”

Katika mahojiano hayo pia, Wema alimuuliza mrembo huyo jinsi watu wanavyomchukulia kama mwanamke ambaye hajatulia.

“Mimi sina mambo mengi, sina mambo mengi kabisa. Kama kuna mtu karibu yangu ana mambo mengi mimi namkata yeye kabisa ili nikwepe yale mambo mengi,” alisema Tueny.

Mrembo huyo amedai safari yake ilianza baada ya kupiga picha na kuanza kufananishwa na Wema Sepetu na ndipo safari yake ya umaarufu ilipoanza.

Amedai baada ya kugundua hivyo aliaendelea kupiga picha na kupost katika mitandao ya kijamii hali ambayo ilimuongezea mashabiki mara dufu.

Katika hatua nyingine Tueny amewataka mashabiki wa muziki kukaa mkao wa kula kwani anakuja na ngoma mpya zakutosha pamoja na kuachia EP na baadae albamu.

Kwa sasa Tuany ana ngoma mbili, Siri pamoja na Ado Ado ambazo zote hazijapata mapokezi mazuri.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents