Burudani

Tunda Man asema yuko mbioni kukamilisha vifaa vya Band yake mpya

Msanii wa muziki kutoka Tip Top Connection, Tunda Man ameweka wazi mpango wake wa kufungua Band ya muziki atakayoitumia pia katika show zake.

Tundaman

Akizungumza na 255 ya XXL ndani ya Clouds Fm, Tunda amesema kuwa anatarajia mpaka mwezi wa sita kila kitu kitakuwa tayari kwa kazi.

“Kitu ambacho nilikuwa na plan nacho muda mrefu lakini nashukuru Chief ameniambia this time yupo tayari kuniletea vitu vya Band, kwahiyo nilichofurahi kwa sasa hivi show zangu kwa mara nyingi sana nitakuwa nafanya na Band, kwa sababu nitakuwa na mtu wa drum na wengine wanaokamilisha band, watu wa back up , kwahiyo nitafanya Band kwa sababu nilihisi nao mashabiki wanataka muziki wa kweli kabisa kuliko nikiimbia CD, kwahiyo nafikiri mpaka mwezi wa sita itakuwa tayari, kila kitu kipo sawa na mpaka jina la Band hivi juzi kati tulikuwa tuna-discuss , lakini nafikiri kila kitu kipo sawa vitu kadhaa vimeshanunuliwa bado vitu kidogo vilivyobaki, vinatakiwa vinunuliwe ili niwe nafanya show za kiukweli,” alisema Tunda Man.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents