Bongo Movie

Mama Kanumba asikitishwa na wasanii pamoja na wadau wa filamu kususia uzinduzi wa kitabu cha Kanumba

Flora Mtegoa, Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba amesikitishwa na wasanii wa filamu pamoja wa wadau wa filamu kushindwa kwenda kumuunga mkono katika shughuli ya uzinduzi wa kitabu cha Kanumba ‘The Great Fallen Tree’, uliofanyika ndani ya ukumbi wa Landmark Hotel, Dar-es-salaam January 10.

kitabu cha Kanumba

Akizungumza kwa majonzi kwenye Take One Show ya Clouds Tv, Mama Kunumba alisema kuwa wasanii ambao walikuja kwenye uzinduzi huo hawakuzidi kumi.

“Nasikitika sana wasanii wa bongo movies wananisikitisha, umoja hawana wana umoja wa hapa (mdomoni) namuunga mkono Steve Nyerere aliyosema yote, kweli hakuna umoja, wewe ukihesabu sidhani kama waliokuja hapa wamefika kumi,” alisema Mama Kanumba.

Katika hatua nyingine Mama Kanumba amewataka wasanii kuwa na umoja kwani kutokuwa na umoja ndio kunasababisha kushuka kwa tasnia ya filamu.
.
“Namuomba Mungu, awaingie, wageuke wawe na umoja wa kweli ili tasnia iende, inashuka kwaajili hawana umoja,” alimalizia mama Kanumba

Pia mwanadada Elizabeth Lulu ambaye ni mmoja kati ya waliokuwepo kwenye tukio hilo alikuwa na machache ya kuzunguza kuhusu uchache wa wasanii na wadau wengine.

“Mimi siwezi kuongelea sana kwa sababu unajua kitu chochote kinahitaji mtu uguswe, kwahiyo siwezi kumlaumu ambaye hajajitokeza labda hajaguswa lakini zaidi na zaidi mimi nashukuru kwa waliofika basi,” alisema Lulu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents